Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2017

SWALAAH

Kuamka tunaamka saa kumi na mbili Kulala ni saa kumi ikipungua masaa mawili Swala kwetu waislamu imekosa wakati na mahali Jambo la uchungu na huzuni kwa kweli Allah Rabbana ametuamrisha nguzo ya kuswali Wenye Elimu wanatuusia kwa nguvu tuswali Kwa waislamu imekuwa jambo la muhali Ndio maana kwenye hii dunia tumefeli Tukikosa biashara tunakuwa wakali Ndugu kwa ndugu tumezidi ukatili Je tunataka hii iwe ndio hali?? Kwa nini Waislamu tunachukizwa na kuswali?? Ibada gani itakufaa usiposwali? Hatukai tukajiuliza haya maswali? Nani hataki maisha mazuri ya sahali Mafanikio yatakuja pindi tutakapoanza kuswali Inawadia mwezi mtukufu Ramadhani Tunatoka kwa mtukufu Sha'abani Tumesahau malengo yetu duniani Tutaacha swala tukimbilie masahani Hayya 'Alal Falaah Tunaitwa kwenye kufuzu Tunaitwa tukamsujudie Allah Mola mtukufu Tumnyeyekee mwenye biashara zetu Tuswali kwa anayesuluhisha matatizo yote TUJIULIZE TENA: TUTAWACHA LI...