Kulala ni saa kumi ikipungua masaa mawili
Swala kwetu waislamu imekosa wakati na mahali
Jambo la uchungu na huzuni kwa kweli
Allah Rabbana ametuamrisha nguzo ya kuswali
Wenye Elimu wanatuusia kwa nguvu tuswali
Kwa waislamu imekuwa jambo la muhali
Ndio maana kwenye hii dunia tumefeli
Tukikosa biashara tunakuwa wakali
Ndugu kwa ndugu tumezidi ukatili
Je tunataka hii iwe ndio hali??
Kwa nini Waislamu tunachukizwa na kuswali??
Ibada gani itakufaa usiposwali?
Hatukai tukajiuliza haya maswali?
Nani hataki maisha mazuri ya sahali
Mafanikio yatakuja pindi tutakapoanza kuswali
Inawadia mwezi mtukufu Ramadhani
Tunatoka kwa mtukufu Sha'abani
Tumesahau malengo yetu duniani
Tutaacha swala tukimbilie masahani
Hayya 'Alal Falaah
Tunaitwa kwenye kufuzu
Tunaitwa tukamsujudie Allah Mola mtukufu
Tumnyeyekee mwenye biashara zetu
Tuswali kwa anayesuluhisha matatizo yote
TUJIULIZE TENA: TUTAWACHA LINI DHARAU KWA MOLA WETU AL-RAHMAN
Comments
Post a Comment